MTENDAJI MKUU TARURA AONGOZA KIKAO CHA MAMENEJA WA MIKOA, AWASISITIZA KUONGEZA UFANISI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI


Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), Mhandisi Victor Seff, amefanya kikao na Mameneja wa TARURA kutoka mikoa yote nchini kwa njia ya mtandao (Zoom call), ambapo wamejadili maendeleo ya utekelezaji wa miradi, changamoto mbalimbali zinazojitokeza na namna ya kuzipatia utatuzi.


Katika kikao hicho, Mhandisi Seff amewataka Mameneja hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uwajibikaji, huku akisisitiza umuhimu wa kuongeza ufanisi katika usimamizi wa miradi yote ya TARURA, ikiwemo ile ya CERC (Contingent Emergency Response Component) inayolenga kushughulikia miradi ya dharura.

No comments