Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe afanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania



Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Grace Magembe, leo Januari 22, 2026 amefanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Tanzania Dkt. Alex Ntale Gasasira. 


Mazungumzo hayo yamelenga kuimarisha huduma za afya nchini hususani wakati wa maandalizi ya utekelezaji wa Mpango wa Bima ya Afya kwa Wote,  Maandalizi ya Mpango Mkakati wa Sekta ya Afya wa Sita (HSSP VI) pamoja na kukubaliana namna bora ya kuimarisha huduma kwa wananchi.


Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali amepokea taarifa kutoka kwa timu ya wataalam wa WHO Kanda ya Afrika iliyowasilishwa na Bi. Chinenyenwa Josephine Henshaw kuhusu tathmini ya uwezo wa Maabara ya Taifa katika upimaji wa magonjwa ya mlipuko. 



Taarifa hiyo imeonesha uwezo mkubwa wa maabara hiyo inayo kidhi vigezo vya kuongezewa idadi na aina ya vipimo vya magonjwa ya milipuko vinavyoweza kufanyika nchini badala ya kusafirisha sampuli nje ya nchi. 


Mwezi Mei,  2025, maabara hiyo ilipata ithibati ya Kitaifa (Accreditation) kutoka shirika la kudhibiti viwango vya ubora wa huduma za Maabara liitwalo SADCAS kutoka nchini Botswana.







 

No comments