BALOZI LUVANDA AZURU NEMC, AIPONGEZA KWA UWAJIBIKAJI WENYE TIJA
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Balozi Baraka Luvanda, amelipongeza Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa uwajibikaji katika kutekeleza majukumu ya kuhifadhi na kusimamia mazingira nchini.
Ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kwanza katika ofisi za NEMC zilizopo Mikocheni jijini Dar es Salaam tangu kuteuliwa kwake, akieleza kuwa lengo la ziara hiyo ni kukutana na watumishi wa Baraza hilo na kuhimiza juhudi za kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya mazingira, ambayo ni mhimili muhimu katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Balozi Luvanda aliwataka watumishi wa NEMC kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uzalendo katika kusimamia rasilimali za mazingira kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Awali, Mkurugenzi Mkuu wa NEMC, Dkt. Immaculate Sware Semesi, alisema kwa mujibu wa Sheria ya Mazingira ya mwaka 2004, Baraza hilo lina jukumu la kusimamia na kulinda mazingira, kufanya tathmini ya athari za mazingira (EIA), kukagua miradi ya maendeleo, kutoa elimu ya mazingira, kudhibiti uchafuzi pamoja na kushauri Serikali kuhusu masuala ya mazingira. Aliahidi kuwa watumishi wa NEMC wataendelea kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ushirikiano ili kufanikisha maendeleo endelevu ya Taifa.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)


Post a Comment