SERIKALI KUIFANYA TANZANIA KITOVU CHA BIASHARA-DKT.YONAZI.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge,Uratibu na Wenye Ulemavu Dkt. Jim Yonazi,amesema Serikali imefanya juhudi mbalimbali za Kisera, Sheria na Kimkakati ili kuhakikisha Tanzania inakuwa kitovu cha biashara Afrika Mashariki na Kati.
Dkt. Yonazi amesema hayo katika kikao cha Kikundi Kazi cha Mazingira ya Biashara cha Baraza la Taifa la Biashara TNBC kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Amesema Serikali imefanya jitihada za kukuza biashara nchini huku akizitaka sekta binafsi kuendelea kushirikiana na serikali.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) Dkt. Godwill Wanga, amesema kikao hicho kimefanyika ili kujadili maendeleo ya biashara nchini.
Amesema kikao hicho kimejadili vivutio ambavyo serikali inaweza kufanya uwekezaji zaidi katika sekta ya afya ili bima ya afya kwa wote itakapoanza iweze kuwa na faida kwa Watanzania.
Post a Comment