AMANI NA UTULIVU NI JUKUMU LA KILA MWANANCHI – KIHONGOSI



Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kenan Kihongosi, amesema kuwa amani na utulivu ni wajibu wa kila mwananchi, akisisitiza kuwa hakuna mbadala wake katika kuhakikisha maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Akizungumza na wanachama wa CCM katika shina namba 12, Kijiji cha Bugurula, Jimbo la Geita Vijijini, Kihongosi ameonya kuwa machafuko yanaposhamiri, kila mtu huathirika kutokana na uharibifu wa mali na kusimama kwa shughuli za kiuchumi.


Ameleza kuwa jamii zilizoelimika haziwezi kujihusisha na vitendo vya kuchoma au kuharibu mali zao wenyewe, hivyo ni muhimu kwa wananchi kulinda maeneo yao na kuhakikisha amani inadumishwa wakati wote.


Aidha, amewataka wananchi kutokubali watu kutoka maeneo mengine kuingia na kuchochea vurugu, akibainisha kuwa vitendo hivyo havina faida yoyote kwa maendeleo ya jamii husika.


Kihongosi amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila mwananchi kushirikiana katika kulinda usalama wa eneo lake ili kudumisha mshikamano na kuendeleza ustawi wa jamii










No comments