CCM YAFAFANUA MFUMOKO WA BEI WA MAFUTA NCHI YAITAKA SERIKALI KUJENGA VITUO VYA GESI
Aidha, amesisitiza ujenzi wa usafiri wa umma wa kisasa, ikiwemo vituo vya kuchaji vyombo vinavyotumia umeme, pamoja na miradi ya kiuchumi inayozalisha bidhaa za kuuza nje, ili kuimarisha uchumi wa ndani na kupungu
pia amebainisha kuwa Chama Cha Mapinduzi kimependekeza hatua nyingine za kudhibiti athari za ongezeko la bei ya mafuta duniani, ikiwemo kuanzisha Mfuko wa Kuhimili Ukali wa Bei za Mafuta, Hifadhi ya Mafuta ya Kimkakati, na Petroleum Hub itakayohakikisha upatikanaji wa mafuta kwa uhakika na kwa bei nafuu.
Aidha, Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitaka serikali kuanza mchakato wa kuhakikisha mafuta ya Petroli na dizeli yanaendelea kupatikana nchini pamoja na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania TPDC kuendelea kuwa kiungo muhimu katika uagizaji wa mafuta nchini kwa kudhibiti hujuma katika sekta ya mafuta hasa kwa njama za kutaka kuchepusha meli za mafuta na kwenda kuuza maeneo mengine.
Kihongosi amesistiza umuhimu wa kupunguza matumizi ya mafuta katika taasisi za serikali, binafsi na umma kwa ujumla, na kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala. “Hii itatusaidia kuwa na uwezo wa kujiendesha kwa nishati mbadala pale changamoto za mafuta zinapotokea,” amesema Kihongosi
Pia, amesema kuwa CCM itaendelea kushirikiana na serikali kuhakikisha hatua zote zinazochukuliwa zinawalenga wananchi na kulinda maslahi mapana ya taifa.
Post a Comment