CHANGAMOTO SEKTA YA AFYA DAR ZATATULIWA KWA WAKATI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila amesema wananchi wanapaswa kutumia fursa zilizopo kuendelea kuimarisha maendeleo yenye lengo la kuboresha maisha yao na ustawi wa jamii kwa ujumla kwa kuwa Serikali imewekeza sana kwenye sekta ya afya.
Mhe. Chalamila amesema hayo leo Aprili 16, 2026 katika Mkutano wa pili wa kimataifa wa shirikisho la jumuiya ya madaktari wa upasuaji wa ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu unaofanyika katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi katika Mkutano huo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Amesema ushirikiano kati ya serikali, sekta binafsi na makampuni mbalimbali ni muhimu katika kuongeza ufanisi na kuchochea mafanikio ya kiuchumi.
Aidha, amesema pamoja na changamoto zilizopo, bado yapo mafanikio makubwa yaliyopatikana ikiwemo kuongezeka kwa mapato kutokana na mikataba mbalimbali ya maendeleo.
Mkuu huyo wa mkoa amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuthamini juhudi zinazofanyika, kusimamia rasilimali kwa uwazi pamoja na kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo madeni ili kuharakisha maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla.




Post a Comment