TPBCA YAKAMILISHA MCHAKATO WA RASIMU YA KATIBA MPYA
Chama cha makocha wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, TPBCA, kimekamilisha mchakato wa kupitia rasimu ya katiba mpya leo jijini Dar es salaam.
TPBCA ilifanya kikao cha kukamilisha mchakato huo ambapo wanachama wa chama hiko ambao ni makocha wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania wameshiriki kikamilifu katika zoezi hilo ambalo limefanyika leo.
Miongoni mwa mapendekezo yaliyokuwepo kwenye rasimu hiyo ni hitaji la makocha kusafiri na mabondia wao popote pale wanapoenda kwenye mapambano, mikataba baina ya makocha na mabondia wao pamoja na masuala mengine yenye masilahi na makocha hao.
Baada ya mchakato huo kikamilika rasimu hiyo itasainiwa na mwenyekiti wa TPBCA, Jafari Ndame na katibu wake Juma Mbogo.
Baada ya rasimu hiyo kusainiwa na viongozi hao wa TPBCA itawasilishwa kwenye Baraza la Taifa la Michezo, BMT, ili ipitishwe na kuwa katiba rasmi ya chama hiko kuanzia mwaka huu wa 2026.
Post a Comment