TRA KILIMANJARO YAPELEKA MSAADA KWA WAGONJWA KCMC
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Kilimanjaro, tarehe 01 Aprili 2026, imeshiriki katika zoezi la kutoa faraja pamoja na mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa mkoani humo, ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii.
Akizungumza baada ya kutembelea wodi ya watoto katika kitengo cha kansa kilichopo Hospitali ya KCMC (Kilimanjaro Christian Medical Centre), Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Bw. James Jilala, akiambatana na menejimenti ya mkoa, amesema kuwa TRA itaendelea kushirikiana na jamii, hususani makundi yenye mahitaji maalum, ikiwemo watoto wanaosumbuliwa na saratani ili kuleta faraja katika jamii.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa KCMC, Prof. Gileard Masenga, ameishukuru TRA kwa kujitoa na kugusa maisha ya watoto hao. Amesema mchango huo ni muhimu kwani unaongeza faraja na kusaidia kukidhi mahitaji yao ya msingi wakati wa matibabu.
Post a Comment