TASAC YASHIRIKI MAZISHI YA BAHARIA ALIYEFARIKI AKIWA KAZINI KATIKA MFEREJI WA HORMUZ
Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC), jana tarehe 21 Mei, 2026, limeshiriki shughuli za mazishi ya baharia Mtanzania, Nahodha Mchama Maregesi Mongu, aliyefariki dunia akiwa kazini katika Mfereji wa Hormuz nchini Iran.
Mazishi hayo yamefanyika katika Makaburi ya Mwisenge, yaliyopo Musoma Mjini, mkoani Mara.
Kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Shirika liliwakilishwa na Mha. Lameck Sondo, Meneja Mafunzo na Utoaji Vyeti kwa Mabaharia.
Wakizungumza wakati wa mazishi hayo, ndugu wa marehemu waliishukuru Serikali pamoja na TASAC kwa ushirikiano na juhudi zilizowezesha mwili wa ndugu yao kurejeshwa nchini kwa ajili ya mazishi.
Nahodha Mchama Maregesi Mongu alifariki dunia tarehe 3 Mei, 2026 katika Mfereji wa Hormuz nchini Iran akiwa kazini ndani ya meli ya kuvuta (tug boat) iitwayo VOLANS, inayopeperusha bendera ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), iliyokuwa ikisafiri kutoka UAE kuelekea Oman.





Post a Comment