WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA KUTEKELEZA VIPAUMBELE SABA 2026/2027.



WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Judith Kapinga, ametaja vipaumbele saba vitakavyotekelezwa katika mwaka wa fedha 2026/2027.


Miongoni mwa vipaumbele hivyo ni 

kuendelea kutekeleza miradi ya kimkakati na ya kielelezo ya viwanda sambamba na kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani kupitia kuboresha mazingira wezeshi ya biashara.


Akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo Mei 22,2026, bungeni jijini Dodoma, Waziri Kapinga amesema Serikali pia itaendelea na ujenzi wa miundombinu ya kongani za viwanda na mitaa ya viwanda kwa ajili ya kusaidia viwanda vidogo na vya kati ili kuongeza uzalishaji na ajira.


Kwa mujibu wa Waziri huyo, Wizara itaendelea kuchochea maendeleo ya viwanda na biashara kupitia ubunifu, matumizi ya teknolojia za kisasa, elimu pamoja na mafunzo ya ujuzi kwa vijana na wajasiriamali.


Ameongeza kuwa juhudi pia zitaelekezwa katika kuimarisha upatikanaji wa fedha na mitaji kwa wajasiriamali na wazalishaji viwandani, kuboresha mazingira ya biashara na kukuza sekta binafsi.


Waziri Kapinga ametaja kipaumbele kingine kuwa ni kuanzisha na kuendeleza vituo vya ubunifu na biashara kwa vijana kwa lengo la kuchochea ukuaji wa uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini.

No comments