WAZIRI MCHENGERWA AKAGUA UJENZI HOSPITALI YA WILAYA MWANGA



Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, leo Julai 23, 2026 amekagua mradi wa ujenzi wa hospitali ya Wilaya Mwanga na mradi wa ujenzi wa chuo cha Veta Mwanga. 


Katika ziara hiyo ya Siku nne, Mhe. Mchengerwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Nurdin Babu, ambapo wamekagua maendeleo ya miradi hiyo inayolenga kuboresha mazingira ya huduma za afya na mikakati ya kuinua nyenzo za elimu nchini.


Aidha, akiwa katika hospitali ya Wilaya Mwanga amepongeza kwa kazi kubwa inayofanywa na Serikali katika sekta mbalimbali katika kipindi kifupi cha Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.


Amewaomba wananchi wa mkoa huo na Watanzania kwa ujumla waendelee kuiunga mkono Serikali katika  miradi mbalimbali inayotekeleza.




















No comments