DC KUBECHA AWATAKA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUFANYA KILIMO NA UFUGAJI KIBIASHARA

Mkuu wa wilaya ya Gairo Mhe.Japhari Kubecha Amewataka Wakulima na Wafugaji katika Wilaya ya Gairo na maeneo mengine kubadili mtazamo na kuanza kufanya Shughuli za kilimo na ufugaji kwa njia ya kibiashara ili kuongeza  kipato na kuchangia Maendeleo ya kiuchumi ,
-
Dc Kubecha ametoa wito huo alipotembelea banda la Halmashauri ya Wilaya ya Gairo katika maonesho ya Kilimo na Uvuvi ya nanenane kanda ya Mashariki yanayofanyika katika viwanja vya Mwl.Julius.k.nyerere ,Manispaa ya Morogoro, 
-
Akizungumza na washiriki wa maonesho wakiwemo wakulima ,wafugaji ,vijana na Wajasiriamali Mhe .Kubecha amesema Serikali ya Awamu ya sita Inayoongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan imeweka mazingira wezeshi kwaajili ya kilimo na ufugaji wa kisasa ,hivyo Wananchi wanapaswa kuchangamkia fursa hizo kwa kutumia maarifa ,Teknolojia na mbinu za uzalishaji. 

Maonesho ya Nanenane kwa Mwaka 2025 yamebebwa na kaulimbiu " chagua Viongozi Bora kwa maendeleo endelevu ya kilimo ,Mifugo na Uvuvi 2025 "

No comments