BEI YA MAFUTA KUPUNGUZA MAGARI MSAFARA WA RAIS DKT SAMIA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza hatua ya kupunguza matumizi ya mafuta serikalini kwa kuanza na ofisi yake, akisema kuanzia sasa viongozi wakubwa watapanda pamoja katika basi moja badala ya kila mmoja kutumia gari lake.


Akizungumza leo Jumatano, Aprili 8, 2026 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma wakati wa kuwaapisha viongozi wapya aliowateua.

“Tunaanza kupunguza matumizi ya mafuta na naanza na ofisini kwangu. Ninapotembea maofisa wote wakubwa wananifuata nyuma na magari yao, kuanzia sasa ninapokwenda kokote, wote nawaingiza kwenye kibasi kimoja,” amesema Rais Samia.

Amesema msafara wake utakuwa na ulinzi wa kawaida, ukiwemo msafara wa polisi (escort) pamoja na gari ya akiba nyuma, lakini idadi ya magari ya viongozi itapunguzwa kwa kiasi kikubwa.

No comments