RAIS DKT SAMIA AZINDUA KITUO CHA BIASHANA NA USAFIRISHAJI AFRIKA MASHARIKI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo amezindua rasmi Kituo cha Biashara na Usafirishaji Afrika Mashariki (East African Commercial and Logistics Centre - EACLC) kilichopo Ubungo, Dar es Salaam, akisema kituo hicho kitakuwa mfano wa ushirikiano wa kibiashara kikanda na kitaleta neema na ustawi kwa nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini.
Katika hotuba yake, Rais Samia amesema kuwa uwekezaji huo utaungana na juhudi za Serikali katika kujenga imani kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa kimataifa ili kuvutiwa kufanya shughuli zao nchini Tanzania.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, amesema idadi ya biashara katika Jimbo la Ubungo imeongezeka kutoka 4,220 mwaka 2020 hadi 8,997 mwaka 2025, ikiwa ni ongezeko la asilimia 113, jambo linaloonesha mafanikio ya kimkakati katika uwekezaji wa maeneo hayo.
Aidha, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, amesema kuwa mradi huo wa kimkakati umewezesha kuingizwa kwa mtaji wa takribani shilingi bilioni 282.huku Wakati wa ujenzi, zaidi ya ajira 2,000 zilitolewa na baada ya kukamilika kwa kituo hicho, ajira za moja kwa moja zipatazo 15,000 zinatarajiwa pamoja na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo
Mradi huo unatajwa kuwa moja ya hatua muhimu kuelekea kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara, usafirishaji na uwekezaji katika ukanda wa Afrika.
Post a Comment