MECHI YA YANGA NA SILVER STRIKERS MASHABIKI KUSHUHUDIA BURE BENJAMINI MKAPA

 


Kikosi cha Yanga kimeingia kambini kwa ajili ya kufanya maandilizi kueleka katika mchezo wa klabu Bingwa Afrika dhidi ya Silver Strikers ya Malawi jumamosi wiki hii.

Meneja wa Habari na mawasiliano   Ally Kamweamesema kikosi hicho kimeingia kambi leo mchana na kinaendelea na maandalizi yake huku wapinzani wao wakitarajiwa kuwali nchini siku ya alhamisi sa mbili usiku.

Yanga inaingia katika mchezo huo wa marejeano wakiwa nyuma kwa goli 1- 0 walipofuingwa ugenini wikiendi iliyopita na kuiweka hatarini nafasi yao ya kufuzu hatua ya makundi kama watashindwa kushinda zaidi ya goli moja wakiwa uwanja wa Benjamini mkapa.

Ally Kamwe amesema amesikia maneno mengi yanaendelea kusema kwenye mitandao ya kijamii kuhusu wachezaji lakini yote yatajibiwa kwa vitendo katika uwanja wa mchezo.

“Nimesoma maneno mengi yanayoandikwa huko mitandaoni, wachezaji wetu wamesemwa sana na niwaambie tu kuwa Yote tumeyasikia, wachezaji wetu wameyasikia yote na wanayafanyia kazi, hatutawajibu kwa maneno, wengi waongea kwa Chuki na Roho mbaya tu, wachezaji wetu watayajibu kwa vitendo yote yanayozungumzwa na Inshaallah Jumamosi majibu yatapatikana.

“Tunajua kuwa wanaotuombea mabaya siyo hao wamalawi, ni hawa hawa tunaoishi nao na kula nao, wakati huu ndiyo wakati wa kuwajua dhahiri maadui zetu, niwaombe wanayanga, raha ya Ngoma ucheze mdundo unaouona siyo unaousikia kwa watu, twendeni kwa Mkapa tukaisapoti timu yetu na Inshaallah tutafuzu hatua ya Makundi” Ally Kamwe


Aidha uongozi wa klabu ya Yanga umekubaliana kuondoa viiongilio katika mchezo huo na kubakisha eneo la VIP A na VIP B kwa ajili ya waalikwa tu.

Amesema ombi hili la kuweka mechi hii isiwe na viingilio lilikuwa gumu sana kukubaliwa kwakuwa viongozi wetu wana mahitaji mengi sana ya kuiendesha timu yetu, lakini kwa kutambua umuhimu wa mchezo huu iliulazimu Uongozi ukubali na kuweka kipaumbele ushindi ambao kila mmoja wetu anauhitaji.

“Tumekubaliana kuwa mechi hii imeondolewa viingilio majukwaa yote isipokuwa jukwaa la VIP A na VIP B yamekuwa Reserved kwa waalikwa maalum ambao ni Wageni wetu pamoja na wanachama wa Yanga wa Black Card.

Kuhusu Kocha mpya, Ally amesema uongozi wa Yanga upo kwenye mchakato mzuri wa kumpata kocha mpya na ndani ya siku tatu hizi mchakato huu utakuwa umekamilika, lakini mchezo wa tarehe 25 utaongozwa na Care taker Patrick Mabedi.

 


 

 

No comments