SHOMARI KAPOMBE KUWANIA TUZO YA CAF YA MCHEZAJI BORA KWA WACHEZAJI WA NDANI

 


Mchezaji wa Simba raia wa Tanzania Beki wa kulia Shomari Kapombe ameingia kwenye Orodha ya wachezaji kumi Bora wanaowania Tuzo za Caf za mwaka kwa wachezaji wa ndani.

Kapombe anaingia kwenye Orodha hiyo akiwania Pamoja na wachezaji wengine kutoka vilabu mbalimbali Afrika ikiwemo mabingwa wa ligi ya mabingwa Afrika Pyramid na Mabingwa wa kombe la shirikisho la CAF Berkane ambao wametawala katika orodha hiyo

Kapombe ni Miongoni mwa wachezaji walioonesha kiwango bora msimu uliopita ambao amechangia kwa kiasi kikubwa klabu yake ya Simba kufika katika hatua ya fainali ya michuano ya kombe la shirikisho la Caf ambapo walipoteza dhidi ya Berkane.


Wengine ambao wametwaja katika orodha ya wachezaji 10 bora ni Pamoja na Ismael Belkacemi (Algeria/Al Ahli Tripoli), Blati Toure (Burkina Faso/Pyramids FC), Issoufou Dayo (Burkina Faso/RS Berkane), Fiston Mayele (DR Congo/Pyramids), Ahmed Samy (Egypt/Pyramids), Emam Ashour (Egypt/Al Ahly), Ibrahim Adel (Egypt/Pyramids), Mohamed Hrimat (Morocco/AS FAR), Mohamed Chibi (Morocco/Pyramids), Oussama Lamlioui (Morocco/RS Berkane)

Shomari Kapombe ni mchezaji pekee anaetokea Tanzania na Afrika Mashariki aliyeingia katika orodha hiyo.



No comments