SIKU YA KUNAWA MIKONO DUNIA, TANZANIA YAHIMIZA "KUWA SHUJAA WA KUNAWA MIKONO"
Tanzania
inaungana na mataifa menguine Duniani katika kuadhimisha siku ya Kunawa Mikono
Duniani. Siku hii hutumika kutoa elimu na kuhamasuisha jamii kudumisha tabia Chanya
ya kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni kama njia Madhubuti na rahisi
katika kudhibiti magonjwa yanayoweza kuenenzwa na mikono iliyochafuliwa na
vimelea mbalimbali vya magonjwa.
Baadhi ya
magonjwa yanayoweza kudhibitiwa kwa kuzingatia unawaji wa mikono kwa maji tiririka
na sabuni mara kwa mara ni Pamoja na ebola, Uviko-19, magonjwa ya macho
kipindupindu, na magonjwa mengine ya kuhara.
Kauli mbiu
ya maadhimisho ya siku ya kunawa mikono kwa mwaka huu ni, “kuwa shujaa wa
kunawa mikono”. Kauli mbiu hii inalenga kuhimiza mtu mmoja mmoja na jamii kwa
mujumla kuhusu umuhimu wa kuzingatia na kudumisha tabia Chanya ya kunawa mikono
kwa nyakati zote muhimu ambzo ni kabla ya kutayarisha chakula, kabla ya kula au
kumlisha mtoto, baada ya kutoaka chooni na baada ya kumsafisha mtoto.
Serikali kupitia
wizara ya afya inatekeleza shughuli mbalimbali za afya Mazingira kama vile kuendesha
kampeni ya Mtu ni Afya ambayo moja ya malengo yake ni kuhamasisha unawaji wa
mikono kwa kutumia maji tirirka na sabuni katika ngazi ya kaya, Taasisi na
maeneo ya umma yenye mikusanyiko ya watu. Kutokana na jitihada zinzofanywa na
serikali ugonjwa wa kipindupindu umedhibitiwa katika mikoa 24 iliyowahi
kukumbwa na ugonjwa huo kati ya 26 ya Tanzania bara na mpaka sasa hakuna
halmashauri yenye ugonjwa huo.
Aidha mfumo
wa wizara wa utoaji wa Taarifa za
magonjwa (DSR) umeonesha idadi ya watu wenye magonjwa ya kuhara wanaokwenda
kwenye vituo imepungua kwa asilimia takribani 76% kwa kipindi cha miaka 5
kutoka wagonjwa 960 956 kwa mwaka 2020 hadi wagonjwa 223 714 kwa mwaka 2025.
Wizara
inaendelea kutekeleza Mradi wa huduma Endelevu za Maji na Usafiw a Mazingira
kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu yam aji, vyoo,na vifaa vya kunawia mikono katika
vituo vya kutolea huduma za afya na shule za msingi nchini. Jumla ya vituo 2,957
na shule 2,125 katika mikoa 25 ya Tanzania Bara vimenufaika.
Ikumbukwe kwa
“Kinga ni bora kuliko Tiba” hivyo wizara inatoa wito kwa mwananchi kuendelea
kudumisha tabia ya kunawa mikono nyakati zote muhimu ili kujikinga na magonjwa
ya kuambukiza.


Post a Comment