SIMBA YAIPANIA NSINGIZINI BENJAMINI MKAPA, WAJA NA "HATUJARIDHIKA TUNATAKA ZAIDI"

 


Kuelekea katika mchezo wa marejeano wa klabu bingwa Afrika kati ya Simba na Nsingizini ya Eswatini, Uongozi wa kalbu ya simba umesema bado haujarishika na matokeo ya mchezo wa mkondo wa kwanza amabo walishinda 3 – 0 ugenini na wakitaka ushindi zaidi katika mchezo ujao ambao utapigwa oktoba 26 katika uwanja wa benjamini Mkapa jijini Dar es salaam

Simba wakuja na kaulimbiu isemayo HATUJARIDHIKA, TUNATAKA ZAIDI ikiwa inalenga kutaka kufahamu nini nini Mwalimu Pantev alimaanisha kusema hajaridhika baada ya kumalizika kwa mchezo uliopita

Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam amesema kwenye mchezo wa kwanza mwalimu aliweka wazi kwamba bado hajaridhika na kiwango cha timu yake, hivyo kipo kitu mwalimu anakitaka na sisi bado hatujakijua.

"Mechi ya Oktoba 26 itakuwa mechi ya kumuona Dimitar Pantev halisi akiwa na ukatili kwenye uwanja wa vita na sisi tunakwenda na kaulimbiu ya HATUJARIDHIKA, TUNATAKA ZAIDI.”



Aidha Ahmed ally amesema kikosi chao kimerejesha hali nzuri ya uchezaji inafanya mashambulizi muda wote na imekuwa simba ya kutisha na kusisitiza mashabiki kuwa hawana sababu ya kukaa nyumbani simu ya mchezo huo.

"Tulikuwa tunapiga kelele kwamba Simba yetu hatuelewi inavyocheza lakini sasa imerejea,  Simba ya kutisha imerejea, Simba ya kushambulia muda wote imerejea sasa unabaki nyumbani kufanya nini. Na haya sio maneno ya kutoka usingizi, haya ni maneno ya kuona inacheza na pale mwalimu anasema uwanja ulikuwa mdogo. Sasa uwanja wa Mkapa anakwenda kwenye uwanja mkubwa, njoo Uwanja wa Mkapa uone Simba ikifanya balaa zito."

"Msiba pekee ndio hauna kiingilio, sisi tunakwenda kwenye starehe lazima kuwe na kiingilio. Huwezi kwenda kumuona mchezaji wa Kombe la Dunia la Vilabu, Seleman Mwalimu, Rushine, Kagoma, Morice, Nangu haiwezi kuwa bure. Siku hiyo sisi tunakwenda kuenjoy, kama una babe wako njoo nae, kama una familia njoo nayo. Hii ni starehe haiwezi kuwa bure."- Semaji Ahmed Ally.

No comments