STANBIC YAZINDUA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA WAKIDHAMIRIA KILA CHANGAMOTO IWEZEKANE


Benki ya Stanbic Tanzania imezindua Wiki ya Huduma kwa Wateja 2025 kwa dhamira moja kuu kufanya kila changamoto ya mteja iwezekane. Timu mbalimbali zimewapokea wateja katika matawi yote nchini na kuanza utekelezaji wa mpango wa siku kadhaa unaolenga kusikiliza, kutatua na kuripoti kwa ushahidi.


Omari Mtiga, Mkuu wa Kitengo cha wateja Binafsi na wateja maalum, Benki ya Stanbic alisema "Kauli ya Mission Possible inamaanisha msaada rahisi na majibu ya haraka ambayo mteja anayahisi mara tu anapoingia tawini Tutawasikiliza wateja wetu, tutachukua hatua, na tutaripoti mabadiliko tunayoyafanya. Hivyo ndivyo tunavyopata imani yao kila siku."


Kauli ya Mission Possible katika Stanbic inategemea nguzo nne kuu: Kujali, Upatikanaji, Kasi, na Uwazi. Katika kipindi cha wiki hii, benki itaendesha dawati maalum la utatuzi (Fix Desk) kwa ajili ya kushughulikia kesi ngumu na kutoa majibu au hatua inayofuata ndani ya siku moja.


Lilian Abdulmalik, Meneja wa Huduma kwa wateja Binafsi, alisema "Hudumal bora inaanza na kujali. Tunawafikia wateja kwa majina, tunawasikiliza bila haraka, na tunatatua tatizo sahihi kwa mara ya kwanza. Hiyo ndiyo Mission Possible kwenye kaunta."


Tuzo ya hivi karibuni kutoka Euromoney kwa Uzoefu Bora wa Wateja inaunga mkono ahadi hii. Tuzo hiyo inaakisi mambo muhimu kwa wateja: majibu ya haraka, mawasiliano ya wazi na ya uaminifu, huruma katika kila hatua ya huduma, mifumo imara, na michakato rahisi inayopunguza usumbufu kwa wateja na wafanyakazi. Stanbic inachukulia haya kama viwango vya kila siku, si


malengo ya muda, na itaendelea kuyaboresha wiki hii. Hilda Kassara, Meneja wa Huduma kwa wateja wakibiashara, alisema "Wamiliki. wa biashara wanathamini kasi na uhakika. Tunatoa muda wa utekelezaji wazi, tunatimiza ahadi, na tunafuatilia hadi kazi ikamilike. Hivyo ndivyo tunavyosaidia. ukuaji wa biashara nchini Tanzania."


Viongozi wa benki watatumia muda wao katika matawi, kukutana na wateja, na kuwashukuru wafanyakazi wanaoleta huduma bora. Timu zitakusanya maoni ya wateja kwa ridhaa yao na kushiriki mafanikio halisi kwenye mitandao ya kijamii, Benki pia itatembelea baadhi ya wateja wa biashara ili kuona huduma kwa vitendo na kusikia mapendekezo ya maboresho yajayo.

No comments