TANZANIA YAPIGA HATUA KUBWA KUKABILIANA NA MAGONJWA YA MLIPUKO
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imezindua rasmi Mradi wa Kuimarisha Uwezo wa Kudhibiti Magonjwa ya Mlipuko na Dharura za Afya (Pandemic Fund Project), hatua muhimu inayolenga kujenga mifumo imara ya afya, kuimarisha miundombinu ya maabara, na kuongeza uwezo wa kitaalam ili kukabili milipuko kwa wakati.
Uzinduzi wa mradi huo umefanyika leo Oktoba 15, 2025, katika Hoteli ya Malaika Beach, jijini Mwanza, ukiongozwa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ambapo mradi huo utatekelezwa kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Wizara ya Mifugo na Uvuvi na mashirika ya maendeleo ikiwemo WHO, UNICEF na FAO, katika ngazi ya taifa hadi mikoa na wilaya.
Kupitia Pandemic Fund, Tanzania imenufaika na msaada wa Dola za Kimarekani Milioni 25 (takriban Shilingi Bilioni 67), fedha zitakazotumika kuboresha mifumo ya ufuatiliaji wa magonjwa, mafunzo ya wataalam wa

Post a Comment