WABUNGE WATEULE WAITWA DODOMA KUHUDHURIA MKUTANO WA KWANZA WA BUNGE LA KUMI NA TATU
Kufutia Tangazo la Rais la kuitisha Bunge lililotolewa kwenye Gazeti la serikali toleo maalum Na. 11(Special Suplement) la tarehe 4 Novemba 2025 Tangazo Na. 647A wabunge wote wanafahamishwa kwamba shughuli za usajili na taratibu nyingine za kuitawala zitafanyika Ofisi za Bunge Dodoma kuanzia tarehe 8 hadi 10 novemba 2025.
Kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa Bunge la 13 kitafanyika tarehe 11 novemba 2025 kama ilivyotamkwa kwenye tangazo la Rais; na shughuli zitakazofanyika katika mkutano huo ni Pamoja na ;-
a) Kusomwa kwa Tangazo la Rais la kuitisha Bunge
b) Uchaguzi wa Spika
c) Kiapo cha uaminifu kwa Wabunge wote.
d) Kuthibitisha uteuzi wa Waziri mkuu;
e) Uchaguzi wa naibu spika na
f) Ufunguzi rasmi wa Bunge jipya utakaofanywa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Utaratibu wa uchaguzi utakaotumika kujaza nafasi ya Spika na Naibu Spika umetangazwa katika Tangazo Na. 1482A na Na. 14824B kwenye Gazeti la serikali toleo maalum Na.11 (Special Supplemente) la tarehe 4. Novemba 2025.
Aidha inasisitizwa kwamba wabunge wateule wote wafike wakiwa wamevaa mavazi rasmi kwa ajili ya zoezi la usaili na upigaji wa picha pamoja na nyaraka zifuatazo;-
A) Hati ya kuchaguliwa /kuteuliwa kwa wabunge
B) Kitambulisho cha Taifa na nakala yake
C) Kadi ya Benki yenye namba ya akaunti ya Mbunge;
D) Cheti halisi cha ndoa kinachotambuliwa na serikali (kwa wenye Ndoa) na nakala yake
E) Vyeti halisi vya kuzaliwa Watoto wenye umri chini ya miaka 21 (kwa wenye watoto/wasiozidi wanne) na nakala
F) Vyeti halisi vya elimu /taaluma vyenye ithibati ya taasisi husika na nakala zake;
G) Wasifu wa Mbunge (Curriculum Vitae)
Imetolewa na katibu wa Bunge
Baraka I. Leonard.
Post a Comment