YANGA KUMKOSA MZIZE WIKI NANE HADI KUMI, WAPELEKA MECHI ZA CAF ZANZIBAR
Kikosi cha yanga kimerejea kamini kwa ajili ya mazoezi ya kujianda na michezo ya ligi kuuu na klabi bingwa Afrika
Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam makao makuu ya klabu hiyo Meneja wa Habari na mawasiliano wa klabu hiyo Ally Shaban Kamwe amesema kikosi hiko kina jiandaa na mchezo dhidi ya Kmc na michezo mingine mitatu ya klabu bingwa Afrika ambayo nayo itachezwa mwezi.
Katika mchezo wa ligi kuu ya NBC Yanga itakipiga dhidi ya Kmc novemba 9 katika uwanja wa Kmc Mwenge jijini Dra es salaam.
Aidha kuhusu mchezo dhidi ya Prisons SC uliyopangwa kuchezwa Dodoma umeahirishwa na tunasubiri tarehe mpya itakayopangwa na Bodi ya Ligi. alisema Ally Kamwe
Pamoja na michezo hiyo Ally Kamwe amesema michezo ya klabu bingwa Afrika itachezwa visiwani Zanzibar
“Baada ya uongozi kufanya Tathimini na kuangalia maslahi mapana ya Klabu yetu, nipende kuwatangazia kuwa mechi zetu zote 3 za nyumbani kwenye hatua ya Makundi, tutatumia uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Amewaomba mashabiki na Wanachama klabu ya Yanga kutoka visiwa vya Pemba na Unguja kujiandaa kuipokea timu na maandalizi ya nguvu kuelekea mchezo wa kwanza wa nyumbani dhidi ya FAR RABAT.
“Wanachama wengine kutoka mikoani tujiandae pia, tupo kwenye kundi gumu lakini tukiwa wamoja, tukiendelea kushiriana kwa umoja wetu tutatoboa". Ally Kamwe
Kuhusu hali za wachezaji husuani mchezaji clement Mzize Ally Kamwe amesema baada ya ushauri wa jopo la madaktari wakishirikiana na benchi la Ufundi na Mchezaji mwenyewe walikubaliana afanyiwe upasuaji.
Maamuzi haya yalikuja baada ya kuona anaendelea kupata maumivu kwenye goti lake kila alipokuwa akirejea uwanjani hivyo mchezaji Clement Mzize atakuwa nje ya uwanja kwa wiki nane mpaka kumi.

Post a Comment