WIKI YA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KUANZA KUADHIMISHA LEO NCHINI TANZANIA
Kauli mbiu
ya mwaka huu ni “Chukua hatua dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza”ambayo inasisitiza
wajibu wa kila mmoja wetu kufikia katika kuchukua hatua za kulinda afya yake na
kusaidia jamii kuwa na maisha yenye ustawi
Magonjwa yasiyoambukiza
ni Pamoja na saratani, kisukari, shinikiza la damu, magonjwa ya moyo, afya ya
akili, figo, selimundu na baadhi ya magonjwa ya njia ya hewa. Takwimu za kidunia
na za hapa nchini zinaonesha idadi ya wagonjwa kuongezeka, inakadiriwa kuwa
zaidi ya asilimia 34 ya vifo nchini Tanzania vinatokana na magonjwa haya.
Kwa kuwa dalili
za magonjwa haya huchelewa kutambuliwa na yanaweza kuzuilika, Wizara ya afya
inawahimiza wananchi kufanya uchunguzi mara kwa mara ili kugundua magonjwa
mapema na kuanza matibabu, kuzingatia mtindo bora wa maisha kwa kula mlo sahihi
yenye virutubisho, kufanya mazoezi angalau dakika 30 kila siku, kuacha matumizi
ya tumbaku na pombe na matibabu ya mapema ili kuzuia na kudhibiti magonjwa
yasiyoambukiza.

Post a Comment