HAPA NDIPO ATAKAPO ZIKWA JENISTA LEO KARIBU NA KABURI LA MUMEWE

Mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Peramiho, Jenista Mhagama unatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Senta B yaliyopo kijiji cha Ruanda, Halmashauri ya Mbinga mkoani Ruvuma, karibu na kaburi la mume wake, marehemu Leonard Mhagama.


Mwili wa marehemu umewasili katika kijiji cha Ruanda tayari kwa ibada fupi ya misa, kabla ya kupelekwa rasmi katika makaburi hayo kwa ajili ya maziko.


Mazishi hayo yanahudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na waombolezaji kutoka maeneo tofauti, ambapo Makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Mchimbi anatarajiwa kuwaongoza waombolezaji.

No comments