MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO NURDIN BABU AMEWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDOMBINU YA BARABARA


Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mhe. Nurdin Babu, amewataka wananchi kutunza miundombinu ya barabara ili idumu na kuleta manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho.


Babu ametoa wito huo Desemba 15, 2025, wakati wa ziara ya wajumbe wa Bodi ya Barabara mkoani humo, iliyolenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayosimamiwa na TANROADS na TARURA.




Akizungumza na wananchi wa Kata ya Kileo, Wilaya ya Moshi Vijijini, Mhe. Babu amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, imesikia kilio cha wananchi wa kata za Kileo, Mabogini na Kahe waliokuwa wakikabiliwa na changamoto ya miundombinu ya barabara, hususan barabara ya Spencon–Mabogini–Kahe.

“Mhe. Rais amesikia kilio chenu katika kata zote tatu na ameleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii. Nawaomba wananchi mtoe ushirikiano wa dhati kwa wakandarasi na muitunze miundombinu hii kwa manufaa ya sasa na ya vizazi vijavyo,” amesema Babu.




Awali, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo, Mhandisi Juma Wambura amesema ujenzi wa barabara hiyo utagharimu shilingi bilioni 7.2 na unatekelezwa na wakandarasi wawili.


No comments