MONUSCO KUSALIA KONGO KWA MWAKA MMOJA ZAIDI

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha azimio la kurefusha muda wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, MONUSCO.


Katika kura iliyopigwa siku ya Ijumaa, Baraza hilo lilipitisha kwa kauli moja kuiongezea muda MONUSCO wa mwaka mmoja hadi Disemba 2026.


Kikosi hicho cha askari karibu 12,000 kilitumwa kwa mara ya kwanza nchini Kongo mwaka 2010 kuchukua nafasi ya ujumbe wa kulinda amani uliokuwa na jukumu kubwa zaidi la kulinda raia na usambazaji wa misaada ya kiutu.


Hata hivyo, hata baada ya miaka 15, Wakongomani wengi wanasema MONUSCO haikutoa ulinzi unaohitajika na raia wakati wa mashambulizi ya makundi ya waasi, na mara kadhaa kumefanyika maandamano ya kuipinga MONUSCO.

No comments