PWANI IMEJIPANGA VIZURI YAFANYA TATHMINI SIKU 100 ZA AHADI ZA RAIS DKT SAMIA SULUHU HASSAN
Mkoa wa Pwani umejipanga kuhakikisha wananchi wa mkoa huo wananufaika moja kwa moja na utekelezaji wa ahadi za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ndani ya siku 100, kwa lengo la kuacha tabasamu na kuboresha huduma muhimu za kijamii.
Akizungumza katika kikao cha tathmini kilichofanyika ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mkuu wa mkoa huo Abubakar Kunenge, amsema yapo maeneo mengine ambayo wanahitaji kuongeza kasi na nguvu, ikiwemo eneo la Bima ya Afya kwa wote.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya taasisi mbalimbali, akieleza kuwa mifumo ya taarifa inapaswa kuoanisha ili kurahisisha utendaji badala ya kila taasisi kuwa na mfumo wake.
Mratibu wa Bima ya Afya kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI, Silvery Maganza, akitoa wasilisho ameeleza kuwa kaya zitakazonufaika na mpango huo ni zile zisizo na uwezo wa kiuchumi zipatazo 900,000, zikiwemo kaya zinazonufaika na mpango wa TASAF.
Amebainisha , utekelezaji wa siku 100 za ahadi za Rais ni wa majaribio, ukianza na makundi maalum yakiwemo watoto, wazee, watu wenye ulemavu na wasio na uwezo, kwa lengo la kutathmini changamoto na maeneo yanayohitaji maboresho kabla ya utekelezaji wa kudumu.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amepata fursa ya kusalimia kikao hicho amewataka wataalamu kuwa wabunifu katika ukusanyaji wa takwimu sahihi za watu wenye mahitaji, akisisitiza kuwa elimu ya kweli ni uwezo wa kufikiri nje ya box ili kupata matokeo chanya.





Post a Comment