RC. CHALAMILA ATAKA CHUO CHA MAGEREZA KUFANYA TAFITI
Awataka wahitimu wa Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania Ukonga Dar es Salaam kuyatumia maarifa na ujuzi walioupata katika utendaji wa kazi zao kama askari magereza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo Disemba 17,2025 wakati wa mahafari ya tatu ya Kozi ya Stashahada ya Sayansi ya Urekebishaji katika chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania Ukonga Jijini Dar es Salaam.
RC Chalamila akiwa mgeni rasmi katika mahafari hayo amepongeza juhudi zinazofanywa na chuo hicho katika kutoa taaluma bora ambapo amekitaka chuo hicho kuendelea kufanya maboresho mbalimbali ili kuwa na mazingira bora ya kufundishia na kujifunzia.
Vilevile ameeleza umuhimu wa chuo hicho kujielekeza katika tafiti ambazo zitasaidia kukiendeleza chuo hicho.
Aidha RC Chalamila amewatunuku Stashahada wanafunzi 44 amabao wamekidhi matakwa ya sheria na kanuni za chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania na kustahili kutunukiwa Stashahada ya Sayansi ya Urekebishaji.
Sanjari na hilo RC Chalamila amemkabidhi zawadi mwanafunzi mmoja Bi Idda P. Danda aliyefanya vizuri zaidi kitaaluma kati ya wanafunzi 44 aliowatunuku Stashahada ya Sayansi ya Urekebishi.
Kabla ya kuhitimisha mahafari ya tatu ya chuo hicho RC Chalamila amepokea ombi la taa za Solar kutoka kwa Mkuu wa chuo ili ziweze kuwekwa katika maeneo mbalimbali ya chuo ambapo amewataka kuleta ofisini kwake mchanganuo wa mahitaji ya taa hizo ili ofisi yake ione namna ya kusaidia

Post a Comment