SPIKA ZUNGU AKUTANA NA BALOZI WA VATICAN NCHINI
Mhe. Mussa Azzan Zungu, Mb. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Vatican Nchini, Mhe. Askofu Mkuu Angelo Accattino, leo tarehe 17 Desemba, 2025 katika Ofisi Ndogo ya Bunge, Dar es Salaam.
Katika kikao hicho, pamoja na masuala mengine, wamejadili kuhusu ushirikiano na uhusiano kati ya Tanzania na Vatican.
Aidha, Mhe. Spika ameeleza kuwa Bunge la Tanzania litaendelea kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi ili kuhakikisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na Vatican unaendelea kuimarika kwa maslahi ya Taifa na wananchi kwa ujumla.

Post a Comment