TUME YA KUCHUNGUZA MATUKIO YA OKTOBA 29 YAKARIBISHA USHAHIDI NA MAONI

Tume iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, ya kuchunguza matukio yaliyotokea siku ya Uchaguzi Oktoba 29, 2025, imetoka taarifa kuwa imeanza rasmi utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Tume za Uchunguzi (Sura ya 32). 


Hivyo inawaalika Wananchi na wadau wote kutoa taarifa, ushahidi, maoni na mapendekezo yatakayo saidia kufahamu ukweli wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2025.


Tume inapokea Maandishi, Picha,  Video, Nyaraka na vielelezo vingine, pia ushuhuda wa ana Kwa ana pamoja na maoni na mapendekezo.

No comments