WATUMISHI WA UMMA WATAKIWA KUSHIRIKIANA KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZILIZOPO KULINGANA NA TAALUMA ZAO
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Rufiji, ambae pia ni Diwani wa Kata ya Shela Abdul Chobo, amewataka watumishi wa umma kushirikiana katika kutatua changamoto zilizopo kulingana na taaluma zao, ili kuiinua jamii katika sekta mbalimbali.
Akizungumza katika kikao cha kwanza na watumishi hao kilichofanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari Mohoro, Chobo ameeleza ,hatua ya kuanza kukutana na watumishi inalenga kuweka misingi ya ushirikiano wa kazi na kupanga mikakati madhubuti ya maendeleo ya kata.
Watumishi na wataalamu wa sekta elimu walitoa mapendekezo ikiwemo kuhakikisha wanafunzi wanapata chakula shuleni ili kuboresha mahudhurio na kiwango cha ufaulu.
Vilevile kuongezeka kwa idadi ya walimu mashuleni, wakiwemo wa kujitolea, ili kupunguza msongamano wa madarasa.
Kwa upande wa sekta ya kilimo, wataalamu wamemshauri kujikita katika kilimo cha kisasa chenye tija, hususan mazao ya biashara kama korosho na mazao ya chakula ili kuongeza uzalishaji.



Post a Comment