RAIS MADURO AWEKWA GEREZA MOJA NA PIDIDI MAREKANI

Rais wa Venezuela Nicolás Maduro anazuiliwa katika Kizuizi cha Metropolitan (MDC) cha Brooklyn.


Inafahamika kwamba atazuiliwa katika kituo hicho kabla ya kukabiliwa na mashtaka ya dawa za kulevya na silaha katika mahakama ya shirikisho ya Manhattan wiki ijayo.


Gereza hilo linajulikana kuwa na mazingira makugumu ya kuishi, vurugu na madai ya usimamizi duni.


Kizuizi cha MDC ndiyo gereza pekee la serikali katika Jiji la New York na kimeshughulikia kesi nyingi za watu maarufu ikiwa ni pamoja na Sean "Diddy" Combs, R. Kelly, El Chapo, mshirika wa Jeffrey Epstein Ghislaine Maxwell.


No comments