MAKAMU WA PILI AFUNGUA SEMINA YA WABUNGE, ASISITIZA UWAJIBIKAJI MFUKO WA JIMBO
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amefungua semina ya wabunge kutoka Zanzibar na kusisitiza umuhimu wa uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo.
Akizungumza Februari 26, 2026, Unguja, amesema mfuko huo umechangia kuboresha huduma za maji, umeme, elimu, barabara na shughuli za kiuchumi, lakini bado kuna changamoto za usimamizi katika baadhi ya halmashauri zilizoibua hoja za ukaguzi.
Amewataka wabunge na watendaji kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika miradi ya maendeleo ili iwe na tija na uendelevu.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhandisi Hamad Yussuf Masauni, amesema semina hiyo itasaidia kuboresha sheria na miongozo ya mfuko huo ili kuongeza uwazi na ufanisi katika matumizi ya fedha za umma.
Semina hiyo imewakutanisha wabunge kutoka majimbo 50 ya Zanzibar, pamoja na viongozi na watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais na Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, kwa lengo la kujadili kwa kina namna bora ya kuimarisha utekelezaji wa Mfuko wa Kuchochea Maendeleo ya Jimbo kwa manufaa ya wananchi.


.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

Post a Comment