SERIKALI KUIMARISHA UWEZO WA WACHIMBAJI WADOGO


Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, amesema dhamira ya serikali ni kuwajengea uwezo wachimbaji wadogo wa madini ili kutimiza malengo yao na kukuza sekta ya madini.

Amesema hatua hiyo inajumuisha kuweka mfumo madhubuti wa usimamizi na kuendelea kutoa leseni katika maeneo yaliyokuwa hayafanyi kazi kwa muda mrefu.

Ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam leo Februari 23, 2026, wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mpango Maalumu kwa Wachimbaji Wadogo wa Madini ya Dhahabu, kati ya Benki ya CRDB na Tume ya Madini.

Waziri Mavunde ameongeza kuwa sekta ya madini ina mchango mkubwa katika ajira na mapato ya ndani, huku akibainisha kuwa zaidi ya watu 18,000 wameajiriwa katika sekta hiyo.

Aidha, ameipongeza Benki ya CRDB kwa kutoa mikopo nafuu kwa wachimbaji wadogo, akisisitiza kuwa uwezeshaji wa wachimbaji wadogo ni njia mojawapo ya kukuza uchumi wa Tanzania.






No comments