SERIKALI KUNUNUA NDEGE NYINGINE NANE MWAKA HUU.
Serikali imesema itanunua ndege nyingine nane mwaka huu ili kuendelea kuimarisha huduma za ndege na kuvutia wawekezaji Nchini.
Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
Msigwa amesema ndege hizo zitasaidia kuendelea kuvutia utalii nchini kwa kurahisisha usafiri wa kuja na kutoka nchini kwa watalii na Watanzania kwa ujumla.
Amesema uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali katika usafiri wa anga na miundombinu yake umevutia kampuni saba kubwa za uwekezaji .
Pia Msigwa amezungumzia mafanikio makubwa yaliyopatikana katika usafiri wa reli nchini.
Amesema zaidi ya abiria Milioni 4.6 wamesafiri kupitia treni ya kisasa SGR.
Ameongeza kuwa usafiri huo umerahisisha huduma mbalimbali na kuongeza pato la Taifa na mwananchi mmoja mmoja .
Pia Msigwa amezungumzia mafanikio yaliyopatikana katika sekta ya bandari nchini.
Post a Comment