SERIKALI YAKABIDHI SIMBA SC KATIBA ILIYOBORESHWA KUENDELEA NA MCHAKATO WA MABADILIKO
Serikali imekabidhi uongozi wa klabu ya simba katiba mpya
iliyofanyiwa maboresho na kuidhinishwa na Msajili wa vyama vay michezo kuwa inaweza kutumia
katika uendeshaji wa klabu hiyo katika mfumo mpya wa hisa.
Akizungumza na waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaa
Msajili wa vyama vya Michezo Abel Ngilangwa amesema hatua iliyokuwa imebaki katika
kuhitimisha rasmi mchakato huo ilikuwa ni kukabidhi kwa uongozi wa simba na
kupokelewa kwa kusaini nyaraka za kukubali marekebisho jambo ambalo limekamilika
na simba wamepokea.
Aidha ameweka wazi marekebisho ambayo yamefanywa katika
katiba hiyo kuwa ni pamoja na kuweka tafsiri sahihi ya simba sports club
campany limited ni kampuni iliyoanzishwa kisheria na itashughulikia shughuli za
kibiashara na kiutendaji za klabu, umiliki wa hisa ukiwa wa ubia kati ya Baraza
la Wadhamini kwa niaba ya wanachama na wawekezaji kwa mujibu wa sheria na
maamuzi halali ya mkutano mkuu.
Pia kuweka bayana kuwa hisa za klabu zitamilikiwa kupitia
baraza la wadhamini kwaniaba ya
wanachama, kuimarisha muundo wa Baraza la wadhamini lenye wajumbe watano na
wasiozidi 7 watakao miliki na kusimamia mali za klabu kwa niaba ya wanachama.
Kuweka wazi kuwa mkutano mkuu ndio chombo chenye mamlaka ya
kuthibitisha Uteuzi na kumuondoa mjumbe wa Baraza la wadhamini pamoja na kuwa
na muundo wa uwakilishi ndani ya Bodi kwa kuzingatia uwiano wa umiliki wa hisa
kati ya wanachama na wawekezaji.
Ngilangwa amesema serikali imeidhinisha katiba hiyo kwa
sababu maelezo hayo yanaendana na sheria ya baraza la michezo la Taifa,
yanaimarisha utawala bora, uwazi na uwajibikaji pamoja na kuzingatia ushauri wa
mwanasheria mkuu wa serikali aliyoutoa kwa klabu ya simba.
Vilevile maboresho hayo hayalengi kunufaisha watu wachache
bali kuweka uwiano wa haki kwa wanachama na wawekezaji, kuondoa changamoto za
kisheria na kiutawala na kuweka msingi thabiti wa usajili, umiliki na usimamizi
wa mali kwa kuzingatia sheria za nchi.
Hata hivyo Ngilangwa amesema serikali inaamini kuwa kupitia
katiba hiyo iliyoboreshwa klabu ya simba itajenga mazingira rafiki kwa
uwekezaji, itaheshimu uwekezaji uliokwisha kufanyika na unaotarajiwa kufanyika
hivyo kuepusha migogoro ambayo serikali haitarajii ijitokeze.
Amesisitiza kuwa sio jukumu la serikali kufanya uamuzi wa
klabu kwenda kwenye aina nyingine ya uendeshaji bali kuidhidnisha marekebisho
ya katiba yanayokidhi matakwa ya sheria na kwamba inajiridhisha kuwa
marekebisho hayo hayaendi kuathiri maendeleo ya klabu, kuvuruga Amani miongoni
mwa wanachama na kuvuruga usalama.
Ametoa wito kwa wanachama wa klabu ya simba na wadau wake
wote kuhershimu maamuzi ya kisheria ili klabu kuendelea kuwa na utulivu
mshikamano na mafanikio makubwa Zaidi








Post a Comment