ALIYEKUWA MBUNGE WA KILWA KUSINI SELEMAN “BWEGE” AFARIKI DUNIA

 


Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini kupitia CUF, Seleman Bungara maarufu kwa jina la Bwege, amefariki dunia leo Jumatatu, Machi 30, 2026, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali iliyopo eneo la Kibada, wilayani Kigamboni jijini Dar es Salaam.


Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na mtoto wake, Hassan Seleman Bungara, aliyeeleza kuwa kiongozi huyo wa zamani alikuwa akiendelea kupatiwa matibabu kabla ya umauti kumkuta.


Marehemu Bungara alihudumu kama Mbunge wa Kilwa Kusini kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 kupitia tiketi ya CUF, ambapo alijulikana kwa mchango wake katika masuala ya kisiasa na maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo.

No comments