BALOZI KAGANDA APOKEA WANAFUNZI WA KITANZANIA WASHIRIKI WA MUN NCHINI ZIMBABWE

Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Mhe.C.P Suzan S. Kaganda, amepokea ujumbe wa wanafunzi 25 pamoja na walimu wao kutoka Shule za Sekondari za Loyola na Mtakatifu Joseph za jijini Dar es Salaam waliowasili nchini humo kwa ziara ya kielimu.

Wanafunzi hao, wakiongozwa na Bw. Joseph Chekube, wapo nchini Zimbabwe kwa ziara ya siku nne kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Model United Nations (MUN) wa mwaka 2026 unaoratibiwa na Chuo Kikuu cha Arrupe (Arrupe Jesuit University).

Akizungumza wakati wa mapokezi hayo, Balozi Kaganda amewashukuru wanafunzi hao kwa kutembelea Ubalozi wa Tanzania na kuwakumbusha kuzingatia maadili mema ya Kitanzania katika kipindi chote cha mkutano huo. Aidha, amewahimiza kuwa mabalozi wazuri wa matumizi ya lugha ya Kiswahili pamoja na kuzingatia masomo yao, akisisitiza kuwa wao ndio taifa la kesho.

No comments