BANDARI FC YAANZA SAFARI KUIFUATA MBEYA CITY
Timu yetu ya Bandari Tanzania Sc, imeanza safari kutoka Jijini Mbeya kuelekea Mkoani Pwani baada ya mchezo wa jana wa CRDB Federation dhidi ya Mbeya City ambapo timu yetu ilipoteza kwa kufungwa magoli matatu kwa bila.
Ofisa Habaru wa Barandi Philipo Chimi amesema Baada ya mchezo huo uongozi ,benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamerejesha nguvu zetu katika michezo yetu ya ligi daraja la pili (First League) ambapo tarehe 14 watamenyana na Nyumbu FC katika uwanja wa Filbert Bayi Kibaha mkoani Pwani.
"Tunawashukuru wadau na mashabiki zetu wote ambao mmekuwa mnatuunga mkono katika mechi zetu tulizocheza kwenye mashindano haya ya CRDB Federation Cup, bahati mbaya tumetolewa lakini tumejifunza mengi ambayo yatatufanya tuwe imara zaidi kwenye ligi"
"Wapinzani wetu sasa wajipange nguvu zetu zote tumerejesha kwenye Lengo Mama kuhakikisha timu yetu inapanda kucheza Championship msimu ujao.
Niwaombe mashabiki mje kwa wingi tarehe 14 pale Kibaha tutatoa burudani na kuchukua alama tatu kabla ya kurejea Nyumbani Nangwana sijaona Mtwara"
Post a Comment