CHUPA 1,795 ZA DAWA TIBA ZENYE ASILI YA KULEVYA ZAKAMATWA
Tani 9 nukta 93 za dawa za kulevya na chupa 1,795 za dawa tiba zenye asili ya kulevya, zakamatwa nchini na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya.
Pia mamlaka hiyo, imeteketeza Ekari 87.5 za mashamba ya bangi.
Aidha, magari 6 na pikipiki 29 zimekamatwa katika operesheni zilizofanyika mwezi Jaruari mwaka huu huku watuhumiwa 151 wakikamatwa kuhusika na uhalifu huo.
Dawa tiba zenye asili ya kulevya, zimekamatwa kwa kushirikiana na maafisa wa kituo cha forodha cha Mutukula, katika basi la abiria la kampuni ya SR Classic linalofanya safari zake kati ya Uganda, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Aidha, dawa hizo zina uwezo mkubwa wa kusababisha vifo kwa haraka kwa mtumiaji, kwani huharibu mifumo ya mwili hasa mapigo ya moyo, mfumo wa fahamu na mfumo wa upumuaji.

Post a Comment