DKT. KIJAJI ASHIRIKI ZIARA YA WAZIRI MKUU DKT. MWIGULU, MBULU.
Wizara ya Maliasili na Utalii imendelea kushiriki ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Lameki Nchemba (Mb), kwa lengo la kukutana na wananchi kwa lengo la kupata uelewa wa pamoja kuhusu uhifadhi endelevu wa Maliasili nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akiwa ameambatana na baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Wizara hiyo, viongozi wa taasisi za Wizara na wataalam, ameshiriki katika ziara hiyo Wilaya ya Mbulu Mkoani Manyara.
Wizara ya Maliasi na Utalii pamoja na mambo Mengine katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Wanyamapori Duniani tarehe 3 Machi 2026 imekuwa ikikutana na wananchi ili kuwasikilisa na kujibu hoja zao kwa lengo la kutatua changamoto zinazohusu uhifadhi na Utalii.

Post a Comment