JAMII YATAKIWA ISHIRIKI KUFICHUA NA KUWABANA WAVUVI HARAMU
Uvuvi haramu umekuwa tishio kubwa kwa uhai wa rasilimali za bahari na ustawi wa mazingira, huku ukichangia kupungua kwa samaki na kuathiri kipato cha jamii zinazotegemea sekta hiyo.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo Mkuu wa Wilaya ya Mafia, mkoani Pwani Aziza Mangosongo, amekemea vitendo vya Uvuvi haramu ambapo ameitaka jamii kushirikiana pamoja na Serikali kufichua wanaojihusisha na Uvuvi huo ili kudhibiti vitendo hivyo .
Akizungumza wakati wa warsha ya kujengea uwezo wadau na taasisi juu ya uhifadhi na usimamizi shirikishi wa rasilimali za bahari, iliyofanyika Machi 18, 2026 Mangosongo amesema Sheria zimetungwa na bunge, wataalam wanavyokwenda kuwakamata wavuvi haramu, sheria iachwe ifuate mkondo wake, jamii iache muhali kwenye mambo ya msingi.
Meneja wa Hifadhi za Bahari na Maeneo Tengefu Tanzania, Emmanuel Sweke, ametoa wito kwa wadau kuendelea kushirikiana ili kuhakikisha rasilimali hizo zinawanufaisha wananchi na Taifa .
Mwenyekiti wa Kijiji cha Juani, Ndugu Mwichande Hassan, amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kutoa elimu kwa wananchi na kuomba yaendelee kufanyika mara kwa mara ili kuongeza uelewa na manufaa kwa jamii.
Warsha hiyo iliandaliwa kwa ushirikiano kati ya Hifadhi za Bahari, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Taasisi ya Sayansi za Bahari, GIZ, ZMT na Chuo Kikuu cha Toliara, imewakutanisha wataalam mbalimbali wakiwemo viongozi wa vijiji na watendaji wa kata.

.jpeg)


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
Post a Comment