KAMATI YA BUNGE YAIPONGEZA SERIKALI KWA UJENZI WA JENGO LA UTAWALA CHUO CHA MAENDELEO YA JAMII TENGERU
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii, imekagua jengo la Utawala la Taasisi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru ikiwa ni sehemu ya ufuatiliaji wa utekelezaji wa miradi inayotekelezwa kwa fedha za Serikali.
Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hawa Mchafu, ameipongeza Wizara kwa usimamizi mzuri wa mradi huo unaotekelezwa katika chuo hicho.
Pamoja na pongezi hizo imeishauri Wizara kuendelea kuimarisha usimamizi wa mradi huo ili kuhakikisha jengo hilo linakamilika kwa wakati na kwa viwango vinavyokidhi mahitaji halisi ya walengwa.
Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum,Mhandisi Maryprisca Mahundi, ameishukuru Kamati hiyo kwa kutembelea chuo hicho na kukagua maendeleo ya mradi huo.
Mahundi amesema Wizara imepokea maoni na ushauri uliotolewa na wajumbe wa Kamati na kwamba wataufanyia kazi kwa haraka ili kuhakikisha ujenzi wa jengo hilo unakamilika kwa wakati na kwa ubora wa viwango vinavyotakiwa.
kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia kuboresha mazingira ya utendaji kazi na kuongeza ufanisi katika utoaji wa huduma za mafunzo katika Taasisi ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru
Post a Comment