KAMATI YA SIASA YA CCM WILAYA YA TABORA YARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA DARAJA KATA YA NDEVELWA.


 

Kamati ya siasa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Tabora ikiongozwa na Mwenyekiti wake Ndg. Mohammed Katete imeridhishwa na kasi ya ujenzi wa mradi wa daraja lililopo katika barabara ya Ndevelwa ikiwa ni sehemu ya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Ilani ya Chama hicho wilayani humo, iliyofanyika Machi 3, 2026.


Akiongea baada ya kupokea taarifa na kukagua mradi huo, Ndg. Katete amesema, Chama Cha Mapinduzi kimeridhishwa na namna mradi huo unavyoendelea ambapo kukamilika kwake kunakwenda kutatua kero ya usafiri kwa wananchi wa Kata ya Ndevelwa na Tabora kwa ujumla, na kutoa pongezi kwa serikali kwa kusimamia vema fedha za miradi zinazotolewa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Naye, Meneja wa TARURA Wilaya ya Tabora Mhandisi Subira Manyama akisoma taarifa ya mradi amesema, mradi huo umegharimu kiasi cha shilingi milioni 391.3 fedha kutoka Kipengele cha Kukabiliana na Dharura (CERC) chini ya     ufadhili wa  Benki ya Dunia, unaotekelezwa na Mkandarasi Valosu Company Limited unatarajiwa kukamilika Aprili 27, 2026.


Aidha, amesema kukamilika kwa mradi huo kutaleta mabadiliko makubwa hususani ukuaji wa sekta ya kilimo na biashara ambapo wananchi watasafirisha mazao na bidhaa sambamba na kuzifikia huduma za kijamii kwa urahisi.









No comments