KIONGOSI AKAGUA DARAJA LA USHETU, ASEMA LITAPUNGUZA HASARA KWA WANANCHI
Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa (CCM), Ndg.Kenan Kihongosi leo amefanya ziara ya kutembelea na kukagua Daraja la Ushetu linalounganisha mikoa ya Tabora, Geita na Shinyanga.
Akizungumza na wananchi mara baada ya ukaguzi huo, Kihongosi amesema kukamilika kwa daraja hilo kutapunguza kwa kiasi kikubwa hasara zilizokuwa zikiwakumba wakulima, wafugaji na wafanyabiashara, hasa wakati wa msimu wa mvua ambapo walishindwa kuvuka kwenda ng’ambo ya pili.
Amesema kwa muda mrefu wananchi wa Ushetu walikumbwa na adha ya mafuriko yaliyokuwa yakikata mawasiliano, hali iliyosababisha kusimama kwa shughuli za kiuchumi na wakati mwingine kupoteza maisha.
Ameongeza kuwa daraja hilo limekamilika ndani ya miaka minne ya awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais , likigharimu Sh bilioni 13.5. Aidha, amesema mradi huo umeenda sambamba na ujenzi wa madaraja mengine mawili ya Kasenga na Ng’hwande.
Amefafanua kuwa, mradi huo kwa sasa uko katika kipindi cha uangalizi ili kuhakikisha unakuwa na ubora unaokidhi thamani ya fedha kabla ya kukabidhiwa rasmi.
Akizungumzia ubora wa daraja hilo, amesema thamani ya fedha inaonekana wazi na kuwataka wananchi kulinda na kutunza miundombinu hiyo ili iwe na manufaa kwa kizazi cha sasa na kijacho


.jpeg)


Post a Comment