MCHENGERWA:TUNADHIBITI NA USIMAMIZI WA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA-NCDs

Waziri wa Afya, Mohammed Mchengerwa, amesema mkakati wa sasa wa serikali katika sekta ya afya unalenga maeneo ya kipaumbele ambayo ni kusaidia kuanzisha na kutekeleza mifumo ya Bima ya Afya kwa Wote ili kupunguza pengo la upatikanaji wa huduma.

Katika mkutano wa nchi washirika wa Mfuko uliofanyika jijini Dar es Salaam, Mchengerwa, amesema serikali itaboresha huduma za mkoba, rufaa na huduma bingwa katika ngazi zote za utoaji huduma, kuimarisha huduma za uchunguzi, kinga, tiba, ukarabati na huduma za kupunguza maumivu katika ngazi zote na kuimarisha afya ya uzazi, mama na mtoto.

Kipaumbele kingine ni kuimarisha kinga, udhibiti na usimamizi wa magonjwa yasiyoambukiza-NCDs, kuimarisha maandalizi na mwitikio wa dharura dhidi ya magonjwa ya milipuko, kuboresha utekelezaji wa tiba mtandao na mifumo ya kielektroniki ya taarifa za afya katika ngazi zote.

Aidha, kusaidia utekelezaji wa tiba asili na mbadala nchini na kuwekeza katika uzalishaji wa ndani wa chanjo, bidhaa na vifaa tiba.

No comments