NAIBU WAZIRI MAGHEMBE ASHIRIKI UZINDUZI WA PROGRAMU YA KUIMARISHA UFUATILIAJI NA USTAHIMILIVU WA SEKTA YA AFYA KWA UMMA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA BARANI AFRIKA


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Dkt. Ngwaru J. Maghembe (Mb), ameshiriki Uzinduzi wa Programu ya Kuimarisha Ufuatiliaji na Ustahimilivu wa Sekta ya Afya kwa Umma na Magonjwa Yasiyoambukiza Barani Afrika (Strengthening Public Health Surveillance and Resilient Knowledge Programme – for NCDs in Africa– SPARK_ ).

Programu hiyo imezinduliwa rasmi na Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar jijini Zanzibar, tarehe 27 Machi, 2026. 

Aidha, Hafla hiyo ya uzinduzi imewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta Afya ikiwa ni pamoja na Kituo cha Kuzuia na Kupambana na Magonjwa Afrika (Africa CDC); Shirika la Afya Duniani (WHO); ECSA- HC; Wizara ya Afya; na Wanazuoni kutoka ndani na nje ya nchi ikiwemo London School of Hygiene & Tropical Medicine_ . 

Washiriki wengine wametoka katika nchi wanachama wa Umoja wa Afrika, Kanda ya Kusini na Mashariki mwa Afrika.

Kwa ujumla programu ya SPARK imelenga kuunganisha jitihada za kupambana na Magonjwa Yasiyoambukiza ikiwemo Moyo, Kisukari, Kansa na Afya ya Akili na jitihada za kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi ili kuimarisha afya ya Bara la Afrika kwa ujumla.

Baada ya uzinduzi huo, watalaamu wataendelea na mkutano wao utakaofanyika kwa siku mbili, Zanzibar tarehe 27 na 28 Machi 2026.

Mheshimiwa Maghembe alishiriki uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb).

No comments