NSSF YAPANDA MITI 600 KATIKA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI MWANZA
Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umepanda miti 600 katika Shule za Msingi Chasubi na Nyakabonga pamoja na Shule ya Sekondari Kayenze wilayani Ilemela, mkoani Mwanza, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa Machi 8.
Zoezi hilo pia lilitumika kutoa elimu kwa wanafunzi na jamii kuhusu umuhimu wa utunzaji wa mazingira pamoja na faida za kujiunga na mifumo ya Hifadhi ya Jamii mapema.
Akizungumza katika zoezi hilo, Meneja wa Wananchi Waliojiajiri wa NSSF, Rehema Chuma, amesema hatua hiyo inaonesha dhamira ya Mfuko katika kuchangia ustawi wa jamii, uchumi na mazingira, huku Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza, Emmanuel Kahensa, akieleza kuwa zoezi hilo limefanikiwa kwa ushirikiano na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) waliotoa miche ya miti.
Walimu na wanafunzi wa shule hizo wameishukuru NSSF kwa zoezi hilo na kuahidi kuitunza miti hiyo ili kuendeleza utunzaji wa mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Post a Comment