"ONGEA NA WAZIRI” KUIMARISHA UWAJIBIKAJI NA UWAZI KATIKA UTOAJI WA HUDUMA ZA AFYA
Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, amesema mfumo wa “Ongea na Waziri” ni daraja muhimu kati ya serikali na wananchi, unaolenga kusikiliza moja kwa moja maoni, kero na mapendekezo ya wananchi.
Mfumo huu, uliozinduliwa rasmi Januari 26, 2026, unalenga kuongeza uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya, na kuhakikisha kwamba maamuzi ya serikali yanaendana na mahitaji halisi ya wananchi.
Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Machi 13, 2026 wakati wa ziara yake katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, jijini Dar es Salaam, ambapo pia alishiriki katika tukio la “Ongea na Waziri” lililowakutanisha watumishi wa afya na wananchi kwa lengo la kusikiliza changamoto na kupokea maoni kuhusu utoaji wa huduma za afya.
Ameongeza kuwa kwa kuanzishwa kwa mfumo huu, serikali inaonyesha dhamira yake ya kutilia mkazo usikilizaji wa wananchi kama msingi wa huduma bora na uwajibikaji, hatua inayochangia moja kwa moja kuboresha sekta ya afya nchini.
Post a Comment